![]() |
| Francis Cheka |
KUPANDISHWA kizimbani
kwa Bondia wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mkanda wa WBF, Francis Cheka,
kumeibua mjadala kwa mashabiki wa mchezo huo huku wengine wakidai ilikuwa
halali yake wengine wakidai ajisafishe kwa kuwaomba radhi.
Cheka ambae ni bingwa wa dunia WBF alipandishwa kizimbani kwa mara
ya kwanza mwishoni mwa wiki na mbele ya hakimu mkazi Said Msuya mkoa wa
Morogoro alisomewa shtaka la shambulio,kudhuru mwili na kujeruhi.
Hata hivyo katika shitaka hilo lililosomwa
na mwendesha mashtaka wa polisi, Aminata Mazengo analodaiwa kulitenda Julai 02
kwa kumpiga ngumi kichwani na tumboni, Bahati Kabanda'masika' yaliyomsababishia
maumivu makali
Mwendesha mashtaka huyo alidai Cheka alitenda kosa la jinai kifungu namba 241 sura ya 25 linalotoa hukumu ya miaka miaka mitano jela endapo atabainika kutenda kosa hilo
Kwa mujibu wa Mazengo,Kabanda aliyekuwa meneja wa baa ya Cheka alipata kipigo hicho kwenye baa hiyo maarufu 'Vijana Social' Sabasaba Manispaa ya Morogoro baada ya kutoridhishwa na mahesabu za mauzo.

Mbele ya hakimu Msuya Cheka alikana
kosa na kudhaminiwa na wadhamini wawili kwa maadishi ya shilingi Mil 1.

No comments:
Post a Comment