Monday, June 2, 2014

WANAKIJIJI watengeneza barabara ili kukabiliana na changamoto ya usafiri inayowakabili


WANANCHI  wa kata ya mabura wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wameamua kutengeneza Barabara zinazozunguka kata hiyo ili kukabiliana na changamoto ya usafiri inayowakabili
.

Akizungumza na Mbiu ya Maendeleo mapema leo Diwani wa kata ya Mabura Meshack Chalo amesema kuwa wananchi wameamua kuchonga barabara hizo kwa kutumia  majembe na mapanga kutokana na adha ya usafiri wanayopata.

Chalo amesema kuwa wananchi wamejitolea kuchonga zaidi ya Kilometa 17 za barabara ya kutoka kijiji cha mabura kwenda mbili yenye  urefu wa kilometa 5, mbili – kagera kilometa 4, Mtumbatu hadi mbili kilometa tano  na mbili – mavungani kilometa tatu na kuongeza kusema kuwa kwa mara ya mwisho barabara hizo Kuchongwa ni mwaka 1974.

Amesema kutokana na Ubovu wa barabara hizo kumepelekea wananchi kushindwa kusafirisha mazao yao kwenda kwenye masoko hali inayosababisha kushuka  kwa uchumi wa kijiji na maendeleo kurudi nyuma.

Aidha Chalo ameleza kuwa kutokana na jitihada zinazofanywa na wananchi wa kijiji  hicho mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi wa saba atahakikisha barabara hizo zinapitika na kwmba anaiomba serikali iwaunge mkono kwa kuchangia ukarabati wa barabara hizo kwani wananchi hao wana haki ya kupata hitaji msaada kutoka serikalini kwkuwa walipakodi wa nchi hii.

No comments:

Post a Comment