SERIKALI ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia
wizara ya Maji imetakiwa kuhakikisha miradi ya maji inakamilkika kwani maeneo
mengi nchini hayana huduma ya maji.
Wito huo umetolewa na wabunge mapema
leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kujadili bajeti ya wizara ya maji kwa kuitaka
wizara hiyo, kukamilisha miradi ya maji kwernye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mbali na hayo Wabunge wameitaka wizara
ya maji kuanzisha mfuko wa maji ili uweze kupunguza urasimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kama ilivyo mifuko ya barabara na umeme.
Mipango ya serikali ni kuwa ifikapo
mwaka 2015 aasilimia 95 ya watu wa vijijini wawe wamepata maji safi na salama hali
inayokwenda kinyume na mikakati na malengo hayo kwani mpaka sasa ni asilimia 65
tu ndio wanapata maji safi na salama
No comments:
Post a Comment