KAIMU mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro
Dokta CHIWEKA ametoa wito kwa wananchi wakiwemo wazee kutoa taarifa
ofisini kwake endapo watatolewa lugha chafu hospitalini mara wanapokwenda
kupata huduma ya matibabu.
Dokta
Chiweka ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na baraza la wazee la mjini Kilosa kufuatia malalamiko
yaliyotolewa na wazee hao kuwa watumishi wa idara ya afya huwanyanyasa
pindi wafikapo hospitalini kupata matibabu.
Akijibu
mnalalamiko hayo,Dokta Chiweka amesema
ameyapokea kwani alikuwa hafahamu kama watumishi wa idara ya afya wanatabia ya
kutoa lugha chafu kwa wagonjwa hospitalini hapo hivyo amewataka kutoa taarifa
ofisini kwa mganga mkuu ili wahusika wachukuliwe hatua .
Kumekuwepo
na malalamiko kuwa baadhi ya watumishi wa ihospitali ya wilaya ya kilosa
wanatabia ya kuwatolea lugha chafu wagonjwa wanapokwenda kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment