MAAFISA ugani wa kilimo katika wilaya ya
Kongwa mkoani Dodoma, wamepongezwa kwa kutoa elimu na kuwahimiza wakulima
katika vijiji mbalimbali vilivyopo wilayani humo kulima mazao
yanayostahimili ukame ilii kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi.
Wakiongea na mbiu ya maendeleo hapo jana wakulima wa vijiji
vya Ngambi , wameeleza kuwa katika msimu wa kilimo kwa mwaka huu wana uhakika
kupata mtama mazao mengi yamatama
kutokana na kusikiliza utaalamu toka kwa maafisa kilimo wa kata na wilaya.
Wamesema , endapo hali ya ushirikiano kati ya wataalamu wa
kilimo na wakulima utaongezeka utasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa chakula
unaoikumba vijiji vingi wilayani humo
mara kwa mara kutokana na wakulima wengi kutozingatia kanuni za
kilimo boracpamoja na baadhi ya wataalamu
kushinda ofisini na kutowatembelea wakulima kwaajili ya ushauri bora.
No comments:
Post a Comment