KAMANDA wa polisi Mkoani Morogoro juzi katika maadhimisho ya siku ya
mtoto alipokelewa na watoto wanaoishi katika mazingira magumu Manispaa ya
Morogoro kwa mabango yenye ujumbe mbalilmbali ukiwemo unaomtaka kuweka kitengo
maalumu cha watoto katika taasisi yake.
Ujumbe huo uliomshawishi
mwakilishi wa kamanda huyo Clemence Matata kutoka dawati la kupinga unyanyasaji
wa kijinsia na ukatili kwa watoto ulikwenda sambamba na laana dhidi ya vitendo
vibaya wanavyotendewa kila kukicha huku kukiwa hakuna hatuia zinazochukuliwa
dhiidi ya wahalifu.
"watoto
tunauwawa,tumekuwa chambo kukidhi haja za kimwili kwa watu wazima wakiwemo
ndugu zetu,ushirikina na yote haya yanafanyika kuwa hatuna wa kututetea kwakua
serikali haitujali...tunaomba serikali itutengenezee mazingira bora ya usalama
na hadhi zetu"alisema Veronica Omari.
Akijibu baadhi ya madai
hayo kwa niaba ya Kamanda,Matata alisema jeshi la polisi limekuwa mstari wa
mbele kupambana na unyanya saji huo kwa watoto na jinsia laikini limekuwa
likikabiliwa na changamoto ya kukosa ushirikiano kwa jamii.
No comments:
Post a Comment