SERIKALI wilayani Rombo mkoani
Kilimanjaro imeunda kikosi kazi maalum cha kukabiliana na wazazi ambao watoto
wao hawajaripoti shuleni kuanza kidato cha kwanza mpaka sasa licha ya kwamba
wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, zoezi ambalo limeelezwa kuanza
kuleta mafanikio makubwa.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo mkuu wa wilaya ya
Rombo Elinasi Palanjo amesema maamuzi ya kuanzishwa kwa kikosi hicho yametokana
na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na
sekondari kidato cha kwanza, kushindwa kuripoti katika shule
walizopangiwa.
Bw Palanjo amesema ,baada ya kufuatilia waliweza kugundua kuwa, jumla
ya watoto 3411 ndiyo walioripoti kati 4332, waliochaguliwa kujiunga na
sekondari kidato cha kwanza,huku watoto 732 hawakujulikana walipo hali
iliyoilazimu serikali wilayani huo kuanza zoezi la kuwasaka watoto hao.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Rombo Bw Judathadeus Mboya,
amesema baada ya serikali kuona kuwa mahakama imeshindwa kuwatia hatiani wazazi
hao ,halmashauri imetunga sheria kwa kutumia kifungu kidogo cha kumlinda
mtoto ambapo baada ya kutunga sheria hiyo, jumla ya wazazi 38 wamefikishwa
katika mahakama za mwanzo zilizoko katika tarafa hiyo.
Wazazi waliokamatwa kwa kushindwa kuwalipia watoto wao ada ya kidato
cha kwanza, wamefikishwa katika mahakama za mwanzo zilizoko katika tarafa hiyo
na kuswekwa rumande kwa muda wa wikimbili kila mmoja
No comments:
Post a Comment