Monday, June 2, 2014

HALMASHAURI nchini zatakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya kuchangia mfuko wa maendeleo ya wanawake



HALMASHAURI nchini zimetakiwa kuendelea kutenga asilimia  kumi ya mapato  ya ndani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Maendeleo ya
wanawake ili kuwawezesha wanawake wengi zaidi kupata mikopo yenye masharti nafuu kupitia mifuko hiyo ikiwemo vikundi vya vijana


Agizo hilo limetolewa jana na  Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa,bwana Abdalalla Bulembo  katika vikao vya Halmashauri kuu ya CCM wilaya za Kilwa,Liwale,Nachingwea na Ruangwa katika ziara yake inayoendelea mkoani Lindi.

Bwana Bulembo amebainisha kuwa maendeleo katika nchi na jamii yoyote yanaanza na wanawake na kwamba mwanamke akiwezeshwa na kuonyeshwa fursa za kujikomboa kiuchumi anaweza kuleta mabadiliko makubwa katika familia na jamii nzima, hivyo ni wajibu wa halmashauri kuwawezesha wanawake kiuchumi ili kutekeleza  sheria ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Katika ziara hiyo ya kukagua utekelezaji wa ilani unaofanywa katika mkoa huo pia  amekagua miradi mbalimbali ya Jumuiya ya wazazi na Vikundi  vya Vijana  na  Jumla ya wanachama 1200 walijiunga na CCM ikiwemo wengine toka vyama vya upinzani







No comments:

Post a Comment