Tuesday, June 3, 2014

WACHOMA mkaa wilayani Kilosa waiomba serikali kuruhusu vibali vya kusafirishia mkaaa vitolewe kwenye serikali ya kijiji


WACHOMA  mkaa kutoka Tarafa ya Ulaya ,wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro wameiomba serikali  kuruhusu vibali vya kusafirisha mkaa vitolewe katika ngazi ya vijiji ili kuweza kuwaongezea kipato ambacho kitawasaidia kukuza uchumi wa wananchi, kijiji na  Taifa kwa ujumla.

Wakiongea na mbiu ya maendeleo wachoma mkaa hao na viongozi wa vijiji na  wachoma mkaa hao na viongozi wa vijiji wamesema kuwa hivi sasa kibali  cha kuchoma mkaa   hutolewa wilayani kwenye ofisi za maliasili pekee kitu ambacho  kinawapa ugumu kupata kutokana na gharama za usafiri kwenda wilaya na umbali uliopo hivyo hivyo kutumia  gharama kubwa kukipata na kusababisha kuuza kwa bei hasara.

Mmoja wa wachoma mkaa Stella Makubi mkazi wa kijiji cha Msimba kata ya Mikumi , amesema wamepata mafunzo kutoka TFCG na Mjumita ya uchomaji mkaa na sasa wanazalisha mkaa mwingi lakini wanashindwa kuuza kwa bei nzuri kutokana na utaratibu wa utolewaji wa vibali vya kusafirishia kutolewa wilayani hali inayosababisha usumbufu mkubwa kukipata hivyo wanaiomba serikali  kuweka utaratibu wa vibali hivyo kutolewa kwenye ngazi za vijiji.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kijiji cha Ulaya Mbuyuni Hamisi Rashidi Mjomba ameyapongeza Mashirika ya TFCG na Mjumita kwa kushirikiana na serikali kuona umuhimu wa kurudisha umiliki wa misitu kwa wananchi na ameomba serikali kuruhusu vibali vya kusafirishia mkaa vitolewe kwenye vijiji.

No comments:

Post a Comment