Tuesday, June 3, 2014

SERIKALI kuwachukulia hatua viongozi wa kijiji na kata wataokaidi amri ya kusoma mapato na matumizi


SERIKALI  imesema itawachukulia hatua viongozi wa vijiji na kata wanaokaidi kusoma mapato na matumizi ya michango ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayochangwa na wananchi katika ngazi ya kijiji.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa  na Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI ) Agrey Mwanri wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu Kristowaja Mtinda wa chama cha CHADEMA aliyetaka kujua hatua zitakazo chukuliwa kwa watumishi hao wanaosababisha wananchi kuacha michango kwa kukosa taarifa.


Mwanri amesema michango katika vijiji na halmashauri inafanyika kwa kibali cha serikali kinachopatikana kwa mkuu wa Wilaya na kwa mujibu wa sheria ni lazima mapato na matumizi yatolewe kwa wananchi kwa kubandikwa ubaoni.

Katika swali la msingi la mbunge wa Tandahimba , Juma Njwayo wa chama cha mapinduzi alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kusaidia halmashauri ya Tandahimba ili kituo cha afya walichojenga kiweze kutoaa huduma bora kwa wananchi.

Amesema Zahanati hiyo ina watumishi watatu , muuguzi mmoja na wahudumu wa afya  wawili, nyumba moja ya mganga na jengo moja la matibabu ya wagonjwa wan je (OPD) ambalo linaendelea kujengwa na limefikia asilimia 85 ya utekelezaji na kusema kuwa katika bajeti ya mwaka 2014/2015 serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 53.6 kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi wa wodi hiyo.


No comments:

Post a Comment