MADAKTARI wa Ukanda wa Ghaza katika
hospitali ya Shuhadaaul- Aqsa wamefanikiwa kuokoa maisha ya mtoto mchanga
ambaye mimba yake ilikuwa na umri wa miezi nane na nusu kutoka katika tumbo la
mama aliyeuawa shahidi kwa hujuma ya ndege za kivita za utawala haramu wa
Israel katika ukanda huo.
Kwa mujibu
wa kanali ya televisheni ya al-Alam, mtoto huyo aliokolewa baada ya kugundulika
kuwa alikuwa angali hai ndani ya tumbo la mama yake, licha ya kwamba mama yake
mzazi alikuwa amekwishafariki dunia.
Habari zaidi zinasema kuwa ndege aina ya F 16 ya
utawala haramu wa Israel iliishambulia nyumba aliyokuwa akiishi Shaimaa na
Ibrahim (wazazi wa mtoto huyo) na kumuua shahidi Shaimaa huku Bwana Ibrahim
akijeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo.
Inaelezwa
kuwa baada ya shambulizi hilo, mama wa mtoto huyo aliangukiwa na vifusi vya
nyumba iliyokuwa imeharibiwa vibaya. Juhudi za waokoaji zilifanikisha kumuondoa
mama wa mtoto huyo ambaye wakati huo tayari alikuwa ameuawa shahidi huku mtoto
akionekana kuwa hai suala lililowafanya kuuharakisha mwili wa mzazi huyo katika
hospitali na kufanikiwa kuokoa maisha ya kichanga hicho.

No comments:
Post a Comment