![]() |
| Mtaaalamu wa kilimo akitoa maelezo viwanja vya nanenane Morogoro |
MAONESHO ya
wakulima yanayofanyika kila mwaka ifikapo tarehe 8, mwezi wa nane iwe chachu ya
kutekeleza mipango kamambe ya limo hasa ule ulioasisiwa na Rais Jakaya Kikwete mkoani Morogoro Maarufu kama
FAMOGATA.
FAMOGATA ni kifupi cha maneno Morogoro kuwa ghala la chakula nchini ni
mpango ulioasisiwa mwaka 2006 na Rais Jakaya Kikiwete lebgo ni kuufanya mkoa wa
Morogoro kuwa ndio mzalishaji mkuu wa chakula nchini.
Wakiongea na Mbiu ya Maendeleo
katika maonesho ya sabasaba ya Mwalimu JK Nyerere maeneo ya nanenane mjini Morogoro,
baadhi ya washiriki wamezitaka serikali na wadau wa kilimo kuhakikisha kuwa
dhana ya Famogata inaendelezwa kwani dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ya
uzalishaji wa chakula kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita, ukame n.k

No comments:
Post a Comment