| Francis Cheka akiwa na meneja wake Mohamed Kingoi |
BONDIA bingwa wa
ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka Novemba 8 anataraji kushuka uwanja wa
Jamuhuri Morogoro kuzichapa na Mkenya Daiel Wanyonyi ikiwa ni maandalizi ya
kuutetea ubingwa wa WBO mwezi Desemba dhiidi ya Mwingereza Daniel Mstosh.
Meneja wa kampuni ya'Life Arts Production'inayodhamini pambano
hilo Mohamed Kingoye na Mratibu wake Peter Kimathi walisema mbali na Mpambano
huo kutakuwa na mapambano mengine matano likiwemo la Cosmas Cheka na Mkenya
Fred Yekese.
"Kwanza Cheka bado ni bondia bora Afrika na Duniani kote
akishikilia mikanda zaidi ya mitano, na mwezi Desemba anataraji kutetea mkanda
mmoja na Mwingereza hivyo tumeamua kumtafutia pambano kumwimarisha"alisema
Meneja Kingoye.
Kwa upande wao Francis na Cosmasi katika mazungumzo hayo na
waandishi wa habari chama cha waandishi wa habari Moropc kwa nayakati tofauti
walisema wamejiandaa kuonyesha burudani ya mwaka kutokana na kutonekana kwa
muda mrefu lingoni.
"namfahamu Wanyonyi vizuri, nibondia mzuri ambae kwa uwezo
wake mabiondia wengi nchini wanamkwepa kuzichapa naoe sasa nataka kuondoa hilo
kwa kumtandika...kumbukeni najiandaa kuchapana na Mwingereza
Mstosh"alisema Francis.
Alikili na mapromota kuwatelekeza mabondia kwa kutowatafutia
michezo alisema imefika wakati wizara ya michezo kuangalia uwezekano wa
kugharimia baadhi ya mampambano ikiwa ni hatua mojawapo ya kuongeza ajira kwa
vijana.
No comments:
Post a Comment