![]() |
| Wafuasi wa Hamas |
UMASHUHURI
wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas umeongezeka huko katika
eneo la Ukanda wa Ghaza lililoathiriwa na vita na katika Ukingo wa Magharibi wa
Mto Jordan, kufuatia mashambulizi ya siku 50 yaliyoanzishwa na Israel katika
eneo hilo.
Kituo cha Sera na
Utafiti cha Palestina kimetoa matokeo hayo ya uchunguzi wa maoni yaliyoonyesha
kuwa, asilimia 61 ya Wapalestina wangemchagua Kiongozi wa Hamas Ismail Hania
kama uchaguzi ungefanyika leo huko Ukanda wa Ghaza. Uchunguzi huo wa maoni umeonyesha
pia kuwa, asilimia 32 ya Wapalestina wangemchagua Mahmoud Abbas Rais wa
serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina.
Utafiti huo wa maoni uliofanywa miongoni mwa
raia wa Palestina vile vile umeonyesha kuwa, asilimia 72 ya Wapalestina
wanaunga mkono mapambano na harakati za muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni
wa Israel, kulinganisha na kile kinachojulikana kama mazungumzo ya amani na
Israel yanayoungwa na chama cha Fat'h cha Mahmoud Abbas na nchi za Magharibi.
Uchunguzi huo wa
maoni ulianza katika siku ya mwisho ya vita vya Israel huko Ghaza yaani tarehe
28 mwezi uliopita na kuendelea hadi katika siku za nne za mwanzo za usitishaji
vita.

No comments:
Post a Comment