SERIKALI ya Libya imeomba msaada wa kimataifa
ilikuzima moto mkubwa unaoendelea kuchoma hifadhi ya mafuta mjini Tripoli baada
ya makombora ya wapiganaji wa Kiislamu kulipua hifadhi ya takriban lita milioni
6 ya mafuta yaliyosafishwa.
Serikali
hiyo changa inayoyumbishwa na mapigano baina ya makundi yanayopinga utawala
uliomrithi Kiongozi wa miaka mingi Maummar Gaddaffi aliyeuawa katika mapinduzi
ya 2011.
Pipa hilo ni
moja ya maghala yanayomilikiwa na kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini Libya -
Brega
Msemaji wa
kampuni hiyo Mohamed Al- Hariri anasema kuwa ikiwa moto huo utasambaa hadi
kwenye mapipa mengine yaliyoko karibu basi itakuwa ni janga.
Serikli ya
mpito nchini Libya imetaka kusitishwa mapigano ili kuruhusu wazima moto
kuendelea na shughuli zao.

No comments:
Post a Comment