Monday, July 28, 2014

WAKULIMA wawataka serikali na Taasisi binafsi kutawanya mbegu bora kwa wakati


Shamba la mbegu ya mpunga la kampuni ya Tanseed ya mkoani Morogoro

WAKULIMA wilaya ya Mvomero,mkoani  Morogoro wameitaka Serikali, Mashirika na Taasi za utafiti nchini kuzalisha  mbegu bora na kuzitawanya kwa wakati kwa wakulima  ili waweze kuzalisha kwa tija.


Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea wilayani humo walisema endapo serikali itasimamia kikamilifu na kuwezesha upatikaji wa pembejeo taifa halitakumbwa na baa la njaa kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya karibuni.

 Aidha Hafeda Jonasi aliongeza kuwa mbali na serikali kutoa pembejeo kwa bei nafuu kwa wakulima kumekuwa na changamoto ya kuchelewa na kuchakachuliwa na watumishi wa serikali.
Mtafiti wa kutoka kituo cha kilimo (mari)Mikocheni Dar es salaam Newton Temu alisema mpango wa taasisi hiyo ni wakulima kutumia mbegu bora za kilimo zinazoletwa na watafiti kulingana na maeneo.

Januari 2014 serikali kupitia wizara ya kilimo chakula na ushirika,kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa kilimo afrika (AATF)  na tume ya sayansi na teknolojia (costech) kupitia mradi wa water efficient maize for afrika na wema-Tanzania walitambulisha mbegu mpya tatu za mahindi.




No comments:

Post a Comment