![]() |
| Viongozi wa Hamas na Palestina |
SERIKALI ya Israel na
wapiganaji wa Hamas wamekubaliana kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la
Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu kuanzia leo asubuhi.
Taarifa ya Israel imesema kuwa raia wa Palestina katika eneo la Gaza ambao walikuwa wameonywa kuondoka katika makaazi yao wasithubutu kurudi na kwamba Israel italipiza kisasi iwapo itashambuliwa.
Bwana Kerry amesema atendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.
Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.
Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30.

No comments:
Post a Comment