Saturday, July 26, 2014

MABILIONI ya JK yashindwa kukopesha wajasiliamali wa Morogoro



Rais Jakaya Kikwete
MFUKO wa Raisi Presidential Trust Fund (PTF) maarufu mabilioni ya JK kanda ya Morogoro umeshindwa kuendelea kutoa mikopo kwa Wajasiliamali na Saccos kwa miaka miwili.

Kushiundwa huko kunatokana na baadhi ya saccos kushindwa kurejesha mikopo baada ya kukopeshwa tangu mwaka 2009-2010.

Meneja wa PTF kanda ya Morogoro Christopher Peter akiitaja saccos ya Ushirikiano Saccos iliyoshindwa kurejesha hata nusu ya deni lake shilingi  Mil 22,128,522 ilizochua mwaka 2009/10 ni miongoni wao.

katika ufafanuzi wake alisema hata uongozi uliotajwa akiwemo mwenyekiti wake Juma Mtumbei ulibadilishwa na kurithiwa na Teobad Mallya aliliyetoroka baadae

hata hivyo aliongeza kuwa mpango wa kuendelea kutoa mikopo kwa saccos uko palepale nakuwa taratibu zimerekebiswa kulazimika kuchambua,kuzisahili na mafunzo na watakao kidhi vigezo watawezeshwa 2014-2015.

Jumla ya fedha kiasi cha shilingi mil 424,laki 9.45 elfu zilikopesha kwa mbalimbali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009-2010.








No comments:

Post a Comment