![]() |
| Tanesco Kihansi, wilayani Kilombero, Morogoro |
WANANCHI wa kijiji cha Mlimba A wilayani Kilombero wameligomea
Shirika la Umeme nchini(TANESCO) tawi la Kihansi kutumia ardhi yao yenye ukubwa
wa ekari 160 kwa madai ya kukiuka makubaliano baina yao.
Tayari wananchi katika eneo wameaza
kugawana kwa matumizi yao binafsi na shughuli za maendeleo baada ya kubaini
kuwa shirika hilo lilitaka kuwatapeli na halina nia njema kwa mujibu wa
makubaliano yao na shirika.
Mbele ya Afisa Tarafa ya Mliba
Jordan Kisonga na kaimu meneja wa Tanesco tawi la Kihansi Idd Mangala kwenye
mkutano kijijini hapo kusaka suluhu baina yao na shirika wanachi hao walisema
muda wa kubembelezana na kuisotea haki yao umekwisha nakuwa sasa ni haki kabla
ya wajibu.
Kwa mujibu wa wananchi hao akiwemo
Jackline Gelvas na mwenyekiti wa kijiji Ramadhani Mkumba wabainisha kwa nia
njema shirika hilo liliomba eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji wa huduma za
kijamii ikiwemo Hospitali na shule mwaka 1994 cha ni kuona wafanyakazi wa
Tanesico kuonekana wakigawiana kinyemela.

No comments:
Post a Comment