Monday, July 7, 2014

WANAWAKE 60 waliotekwa na BOKO Haramu watoroka


Mabint waliotekwa na kikundi cha Boko haramu

TAARIFA kutokaKaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo waliotekwa nyara mwezi jana na Boko Haram wamekwepa.

Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa nyara mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa Kaskazni Mashariki mwa jimbo la Borno.
Serikali ya Nigeria imeitisha uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
Hali ya usalama  ni  mbaya  mno  miundo mbinu duni ikichangia kuifanya hali ngumu kuweza kufikia maficho ya kundi hilo na pia kubaini idadi ya wasichana waliotoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi.
Maafisa wakuu hata hivyo bado hawajaweza kuthibitisha kukwepa kwa wasichana hao.
Wakati huohuo hapajakuwa na taarifa zozote kuhusu wasichana 200 waliotekwa nyara katika shule ye mabweni ya Chibok mwezi Aprili.
Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi ya

No comments:

Post a Comment