Monday, July 7, 2014

KENYA yaimarisha usalama kufuatia maandalizi ya mkutano wa upinzani


Raila Odinga akiwa mkutanoni

USALAMA umeimarishwa nchini Kenya huku upinzani ukijiandaa kwa mkutano mkubwa wa kisiasa ambao wameutaja kama kumbukumbu kwa mkutano na harakati za Saba Saba.

Mkutano huu umeandaliwa na kiongozi wa upinzani CORD Raila Odinga ambaye pia alikuwa waziri mkuu wa zamani na washirika wakubwa
Polisi wameanza doria katika Bustani ya Uhuru Park ambako mkutano huo utafanyika pamoja na maeneo mengine ya mji mkuu Nairobi.
.Muungano wa CORD unatarajia mkutano huo kuwa mkubwa kuliko yote iliyowahi kufanyika nchini humo na kuongeza kuwa utalenga kushauriana na wakenya kuhusu hali ya nchi hiyo.
Pia wanasema kuwa lazima serikali ikubali kufanya mazungumzo nao ili kutafuta suluhu kwa matatizo yanayoikumba nchi hiyo ikiwemo kuzorota kwa usalama , uchumi, ukosefu wa ajira na mfumko wa bei.
Raila anatarajiwa kutoa hotuba na mapendekezo yake kwa serikali ambayo itayawasilisha baadaye.

No comments:

Post a Comment