![]() |
| RAIS Peter Mutharika wa Malawi |
RAIS Peter
Mutharika wa Malawi
amesema kuwa, umasikini ni adui mkubwa zaidi nchini humo.
Akizungumza kwenye sherehe za kutimia miaka 50
ya uhuru wa nchi hiyo, Rais Mutharika amesisitiza kuwa serikali yake inalipatia
kipaumbele suala la kupambana na umasikini. Rais wa Malawi ameongeza kuwa, kutopiga
hatua za kimaendeleo na utegemezi wa misaada ya madola ya kigeni, ndiyo mambo
makuu mawili yaliyodumaza uchumi wa nchi hiyo.
Matamshi ya Rais wa Malawi
yanatolewa katika hali ambayo, takwimu rasmi zinaonyesha kuwa, karibu nusu ya
wananchi wa nchi hiyo wanaishi chini ya mstari wa umasikini, huku nchi hiyo
ikigubikwa na kashfa ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

No comments:
Post a Comment