![]() |
| Wauguzi hospitali ya Morogoro |
MWANAMKE Faustina Sezali(38)wa kijiji cha
Lukuyu Tarafa ya Mgeta wilayani Mvomero amenusurika kufa baada ya kujeruhiwa
kwa panga na mtu anayedaiwa kuwa ni mume wake kwa ajili ya ugomvi wa kugombea
mali.
Faustina
akizungumza kwa taabu katika hospitali ya rufaa mkoani Morogoro alipolazwa
akiugulia majeraha mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani na mgongoni
alimtaja aliyemjeruhi wakigombea mali kuwa ni Rogasiani Jeremiasi.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dr.Ritta Lyamuya ameeleza
kuwa hali ya majeruhi inaendelea vema baada ya kupata huduma ya kwanza.
Hata hivyuo
jeshi la polisi limekili kupata taarifa ya Mwanamke huyo nakuwa anaendelea na
matibabu katika hoispitali hiyo wakati jeshi linamsak mtuhumiwa wa tukio hilo.

No comments:
Post a Comment