![]() |
| Makombora katika mji wa Tel Aviv |
MAAFISA wa
Palestina wanasema kuwa watu kumi na saba wa familia moja wameuawa baada ya
makombora ya Israel kuharibu nyumba moja ya ghorofa tatu ya mkuu wa polisi wa
Hamas.Tayseer Al-Batsh anadaiwa kujeruhiwa
katika shambulizi hilo.
Mashambulizi hayo yanajiri baada ya
wapiganaji wa Hamas kurusha makombora ya masafa marefu katika miji ya Israel
ikiwemo Tel Aviv.
Maafisa wa Israel wanasema kuwa
makombora mawili ya Roketi yalirushwa kutoka lebanon lakini yakaanguka katika
eneo lililo wazi kazkazini mwa Israeli.
Na katika hatua ya kulipiza kisasi
,Israel ilirusha makombora nchini Lebanon na kuzidisha hofu kwamba huenda mzozo
huo ukapanuka.
Takriban raia 150 wa Palestina
wameuawa katika mashambulizi hayo huku ikiwa hakuna vifo vyovyote
vilivyoripotiwa nchini Israel.

No comments:
Post a Comment