Sunday, July 13, 2014

UKAME waathiri uzalishaji wa mahindi Kibaigwa


Wakulima wakiuza mahindi katika soko la Kibaigwa

WAKULIMA mahindi katika wa mji mdogo wa Kibaigwa wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma wameonesha hofu yao ya kushuka kwa uzalishaji wa mahindi katika vijiji mbalimbali vinavyozunguka mji huo kutokana na kuongezeka kwa ukame katika eneo hilo.

Wakiongea na Mbiu ya Maendeleo  wakulma hao wamesema hali ya ukame inazidi kuongezeka na uzalishaji wa mahindi unashuka kila mwaka hivyo ni vyema kwa wataalamu wa kilimo sanjari na wale wa mazingira kutupia jicho hali hiyo ili kunusuru maisha ya wananchi wa Kibaigwa na vijiji vyua jirani .
Wamesema, serikali imejenga soko kubwa la mahindi katika mji huo mdogo , lakini hawana budi kutambua kuwa, ukame unaosababishwa na mabadilikoya tabia nchi yanathiri sana uzalishaji wa zao la mahindi.

No comments:

Post a Comment