Friday, July 11, 2014

UHURU kenyata awaalika futari mabalozi wa nchi za kiislamu


Rais Uhuru Kenyata kushoto na balozi wa Iran nchini Kenya kushoto  Bwana Malik Husein

RAIS  Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliwaalika katika dhifa ya futari mabalozi Waislamu walio nchini humo wakiwakilisha nchi za Kiislamu za Afrika, Asia na Mashariki ya Kati.

 Katika dhifa hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya Rais mjini Nairobi, Rais Kenyatta alisema Kenya inaweza kujifunza mengi kutoka nchi za Kiislamu kwani zinakabiliana na changamoto ambazo hivi sasa Kenya inakabiliana nazo.
Alisema ugaidi na vijana kupewa mafunzo yenye misimamo mikali ni changamoto kubwa katika maelewano ya kitaifa. Rais Kenyatta amesema kuna haja ya Wakenya na jamii ya kimataifa kuungana kupambana na ugaidi na vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vimechukua sura ya kimataifa.
Katika kikao hicho, Rais wa Kenya aliunga mkono pendekezo la kuundwa jopo la mabalozi Waislamu ambao watashirikiana na serikali yake katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili nchi hiyo. Balozi wa Morocco nchini Kenya Bw. Abdelilah Benryane ambaye alizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake alimhakikishia Rais Kenyatta kuwa wamekutana baada ya kubaini kuwa changamoto za usalama zinahitaji umoja na ushirikiano. Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya Bw. Malik Hussein Givzad ni kati ya wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu walioshiriki katika dhifa hiyo ya futari.

No comments:

Post a Comment