![]() |
| Wananchi nchini Afrika ya kati wakihama nchini humo |
SHIRIKA la
kupigania haki za kibinadamu lenye makao yake mjini Washington Marekani Amnesty
International limewataja watu 20 inayowatuhumu kwa kuendeleza mauaji ya kimbari
katika jamhuri ya Afrika ya kati CAR.
Viongozi wa kadhaa wa makundi ya waasi pamoja na marais wawili wa zamani wamo katika Orodha hiyo ambayo Amnesty International inasema ndio wanaochochea kufadhili na kuendeleza mauaji ya halaiki nchini humo.
Aliyekuwa rais wa taifa hilo Francois Bozize aliyeng'olewa madarakani na kundi la wapiganaji wa Seleka chini ya uongozi wake Michel Djotodia, mwezi Marchi mwaka uliopita pamoja na Djotodia mwenyewe wametajwa.
Djotodia aliyeongoza makundi ya waislamu wachache(Seleka) alishurutishwa kunga'atuka madarakani na viongozi wa mataifa jirani mapema mwaka huu, lakini kuondoka kwake kukaibua changamoto nyengine kwani sasa makundi ya wapiganaji wafahamikao kama Anti-Balaka walianza kuwavamia na kuwauwa Waislamu ambao walidaiwa kuwaunga mkono wapihanaji wa Seleka.

No comments:
Post a Comment