WATU 300 waliokuwa wamejihami wamevamia kijiji cha
Pandanguo katika Kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya.
Chifu wa eneo hilo Karisa Charo
Karisa, anasema kuwa shule na nyumba nne ziliteketezwa katika mashambulizi hayo
yaliyofanywa usiku wa kuamkia leo ikiwemo shule moja ya msingi.
Duru zinaarifu kuwa washambuliaji
hao walifanya uvamizi saa tatu usiku na kuiba bunduki sita kutoka kwa polisi wa
akiba.
Walivamia msikiti ambako polisi hao
wa akiba walikuwa wanasali. Mmoja wa polisi hao aliyeponea kifo aliambia waandishi
wa habari kuwa waliambiwa wachague kati
ya mauti na bunduki zao.
Mnamo mwezi Juni watu watano
waliuawa katika eneo hilo la Pandanguo ambalo liko umbali wa kilomita 30 kutoka
Mpeketoni ambako mashambulizi mengine yaliwaacha watu zaidi ya sitini wakiwa
wameuawa.
Mashambulizi ya Kwanza yaliyofanyika
mjini Mpeketoni, yalisemekana kufanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab
ingawa serikali alilalaumu wanasiasa kuyachochea mashambulizi hayo.

No comments:
Post a Comment