![]() |
| Mkulima wa vitunguu akiandaa shamba |
WAKULIMA wa zao
la kitunguu katika vijiji vya Msosa na Mtandika wilayani Kilolo mkoa wa Iringa , wanakabiliwa
na changamoto ya miundo mbinu ya kisasa ya umwagiliaji
.
Wakiongea na mwandishi wa mbiu ya Maendeleo katika vijiji
hivyo hivi karibuni , baadhi ya wakulima wamesema kuwa, msimu wa uandaaji wa
mashamba ya kwaajili ya kilimo cha vitunguu umeanza lakini hali ya miundo mbinu
yaumwagiliaji imechakaa kiasi cha kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo.
Wamesema miundo mbinu ya umwagiliaji katika eneo hilo imeharibiwa
na mvua za masika zilizopita hivyo ni vyema wadau na serikali kuwasaidia
kuboresha ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

No comments:
Post a Comment