Thursday, July 10, 2014

NI ARGENTINA na UJERUMAN fainali za kombe la dunia




Wachezaji wa Argentina wakishangilia ushindi
ARGENTINA imejikatia tikiti ya kufuzu kwa fainali yake ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo itachuana Ujerumani.
Argentina ilikuwa imetoka sare tasa baada ya muda wa kawaida na ule wa Ziada na hivyo kulazimu mechi hiyo kuamulia kwa mikwaju ya penalti.
Kipa wa Argentina Sergio Romero ndiye aliyekuwa nyota katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwaju miwili na kuipa Argentina Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Uholanzi.

No comments:

Post a Comment