Thursday, July 10, 2014

RAIS wa Somalia awafuta kazi maafisa usalama



 
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamud 
RAIS Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amewafuta kazi wakuu wa jeshi la polisi na idara ya upelelezi ya nchi hiyo kufuatia shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa kundi la al Shabab dhidi ya ikulu ya Rais mjini Mogadishu.
Rais wa Somalia pia amemteua mkuu wa zamani wa upelelezi Khalif Ahmed Ereg kuwa Waziri mpya wa Usalama wa Taifa.


Mabadiliko hayo yamefanyika baada ya wapiganaji wa kundi la al Shabab kushambulia ikulu ya Rais wa Somalia siku ya Jumanne ambapo watu kadhaa waliuawa.
Shambulizi la Jumanne iliyopita la al Shabab dhidi ya ikulu ya Rais wa Somalia mjini Mogadishu si kwanza kufanywa na wapiganaji hao. Mwezi Februari mwaka huu wapiganaji wa al Shabab waliokuwa na sare za jeshi walishambulia ikulu hiyo wakiwa na gari lililokuwa na mabomu na kuuawa wote. Mwezi Mei pia wanamgambo wa al Shabab walishambulia jengo la Bunge la Somalia wakati wabunge walipokuwa katika kikao bungeni hapo. Walinzi na maafisa kadhaa waliuawa katika shambulizi hilo.

No comments:

Post a Comment