Swala la vimelea hivyo kujificha kwa
uboho si jambo geni, lakini kundi la wanasayansi wakiongozwa na Profesa
Matthias Marti katika idara ya Afya ya umma kule Harvard, Boston, walifichua
hasa ambako vimelea hivyo hujificha na kutoa maonyesho.
Uzinduzi huu una umuhimu mkubwa kwa
misingi kuwa umeleta ujuzi unaohitajika sana na huweza kupelekea kuundwa kwa
dawa na kinga mpya za kukabiliana na vimelea hivyo ili kuzuia maambukizi.
Kwa mujibu wa wanasayansi huko
Harvard, uchunguzi huu uliochapishwa na jarida la kisayansi la Science Translational
Medicine, umeongeza ujuzi wa kibayologia utakaotumika kuchunguza ugonjwa wa
Malaria hata zaidi.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni
na Shirika la afya duniani, zinapendekeza kuwa Malaria ilisababisha vifo laki
sita mwaka wa 2012, na takriban asilimia tisini ya vifo hivyo vilitokea Afrika.

No comments:
Post a Comment