![]() |
| Mgonjwa wa Ebola akipata matibabu |
AFISA wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) amefariki dunia kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola huko nchini Nigeria.
Jumuiya hiyo imetangaza kuwa, ina masikitiko makubwa kwa kufariki dunia afisa wake Jatto Asihu Abdulqadir aliyekuwa akihudumu katika ofisi yake ya Lagos na kwamba mhanga huyo wa Ebola ni miongoni mwa wasaidizi wa mjumbe wa Liberia kwenye mkutano wa kanda uliomshirikisha Bw.
Partrick Sawyer aliyefariki pia kwa ugonjwa huo tarehe 25 mwezi uliopita.
Agosti 11 jumuiya ya ECOWAS ilitahadharisha kwamba mfumuko wa ugonjwa wa Ebola unatishia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi na kutoa wito kwa nchi wanachama kusaidia kupambana na mfumuko wa ugonjwa huo.
Hakuna tiba ya Ebola na ugonjwa huo husababisha homa inayoambatana na kuharisha, kutapika na mwili kuvuja damu.

No comments:
Post a Comment