![]() |
| Wakimbizi nchini Iraq |
RAIS wa Ufaransa Francois
Hollande ametangaza kuwa taifa lake litawahami wapiganaji WaKurdi
iliwakabiliane na wapiganaji wa Islamic State kaskazini mwa Iraq.
Kulingana na taarifa katika vyombo vya habari vya Ufaransa ,Rais Hollande amepata ruhusa kutoka kwa mamlaka nchini Iraq kuendelea mbele na mpango huo mahsusi wa kuidhibiti Islamic State.
Wapiganaji wa kikurdi wamekuwa wakipiganaji na wapiganaji wa wanamgambo wa Islamic state ambao wameunda himaya yao kaskazini mwa Iraq pamoja na sehemu za Syria.
Mapigano hayo yamesababisha kutokea kwa maelfu ya wakimbizi katika maeneo hayo Kaskazini mwa Iraq

No comments:
Post a Comment