![]() |
| Wachezaji wa Azam Fc wakishangilia goli |
MASHINDANO ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati
maarufu kama kombe la Kagame yanaendelea mjini Kigali.
Timu ya Azam Fc ya Tanzania imetoka
sare ya kufungana magoli 2 na Atlabara ya Sudan Kusini katika katika mashindano
ya kombe la Kagame .
Mechi ilichezwa katika uwanja wa
Nyamirambo jijini Kigali.
Azam wameongoza mchezo na kumaliza
kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa goli 1 lililotiwa kimiani na mshambuliaji
Borou kunako dakika ya 44.
Goli hilo lilikombolewa na
mshambuliaji Thomas kunako dakika ya 48 kabla ya Martin Bonny kufunga goli la
pili la Atlabara kunako dakika ya 54
Azam imesubiri dakika ya 85 kumuona
mshambuliaji wake Kavumbagu akirudishia matumaini ya angalau kupata alama moja.
AZAM inaongoza kundi la A ikiwa na
alama 5 ikifwatiwa na Rayon Sport ya Rwanda yenye alama 4.

No comments:
Post a Comment