KIKAO cha dharura cha kamati ya pamoja ya uratibu ya nchi wanachama
wa harakati ya nchi zisizofungamana na siasa za upande wowote (NAM), kundi la
77 pamoja na China kimefanyika chini ya uwenyekiti wa Gholam-Hossein Dehqani,
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa.
Kikao hicho cha dharura kimefanyika kufuatia
kuendelea kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na
ulinzi wa Ukanda wa Ghaza sambamba na kuibuka maafa ya kibinadamu katika eneo
hilo.
Iran
imeitisha kikao hicho katika juhudi za kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni
huko Ghaza.

No comments:
Post a Comment