RAIS wa Misri,
Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa pendekezo la nchi yake la kusitisha mapigano
ndio suluhu nzuri kabisa ya kumaliza umwagaji damu huko Gaza.
Rais Sisi aliwaambia waandishi wa
habari kwamba hakuna suluhu nyengine mbali ya mpango wa Misri.
Msemaji wa Hamas alieleza kuwa
ujumbe wa Wapalestina utawasaili Cairo hii leo.
Waakilishi wa Marekani, Qatar na
Uturuki piya wanatarajiwa kushiriki katika mazungumzo hayo ingawa haijulikani
ikiwa Israil itatuma ujumbe Jumamosi.
Wakuu wa matibabu wa Gaza wanasema
Wapalestina zaidi ya 200 wameuwawa katika mashambulio ya makomboya ya Israil
tangu Ijumaa, baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuvunjika.

No comments:
Post a Comment