![]() |
| Ndege ya shirika la Emirates |
SHIRIKA la Ndege
la Falme za Ghuba, Emirates, lenye makao yake Dubai, limesimamisha kwa muda
safari za ndege za kwenda Guinea kwa sababu ya ugonjwa wa Ebola ambao umeuwa
zaidi ya watu 700 Afrika magharibi mwaka huu.
Katika tovuti yake Emirates imesema
haiwezi kutia hatarini afya ya abiria na wafanyakazi wake.
Ijumaa, Margaret Chan, mkurugenzi wa
shirika la afya duniani, WHO, alisema virusi vya Ebola vinatapakaa haraka zaidi
kushinda juhudi za kuvidhibiti.
Homa ya Ebola ilianza Guinea na
kutapakaa nchi jirani za Sierra Leone na Liberia.
Mashirika mawili ya ndege ya Afrika, (Arik Air,
ya Nigeria, na ASKY ya Togo,) yameshatangaza kuwa yamevunja safari

No comments:
Post a Comment