![]() |
| Madaktari wakiwa kazini nchini Sirraleone |
MWENYEKITI wa
Halmashauri ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, ametoa wito kwa nchi za
Afrika na duniani kote kushirikiana kuzuwia ugonjwa wa Ebola uliosambaa Afrika
Magharibi, usitapakae kwengineko.
Shirika la Afya Duniani, WHO,
linakisia kuwa watu kama 960 wamekufa kutokana na Ebola huko Guinea, Sierra
Leone, Liberia na Nigeria.
Nkosazana Dlamini-Zuma alisema nchi
za Afrika zinataraji kuunda kitengo cha pamoja kupambana na ugonjwa huo:
"Nchi za Afrika zimefikia
uamauzi kuwa tunataka kuanzisha kitengo cha kudhibiti magonjwa.
Na tutafanya kazi pamoja na
washirika wetu.
Marekani imekwishasema kuwa iko
tayari kushirikiana nasi, lakini siyo pekee.
Lazima tushirikiane sana nashirika
la afya Duniani WHO

No comments:
Post a Comment