![]() |
| Waelimishaji kuhusu ugonjwa wa Ebola nchini Liberia |
LIBERIA imetangaza hatua za dharula dhidi ya ugonjwa
wa Ebola kufuatia kasi kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Rais wa Liberia Hellen Sirleaf
amesema nchi yake kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ugonjwa huo huku baadhi ya
wananchi wakiwa na uelewa mdogo kuhusiana na hatua za kujikinga na ugonjwa huo.
Rais Sirleaf Johnson amelaumu
ukosefu wa elimu na umaskini kama chanzo kikubwa cha maabukizi ya Ebola
Amesema baadhi ya shughuli za
kijamii zimeahirishwa kwa muda ili kuepusha uwezekano wa watu kuambikizwa
virusi vya Ebola.
Hatua hiyo ya Liberia inakuja huku
wataalamu wa afya toka shirika la afya Ulimwenguni WHO wakikutana Geneva,
Switzerland, kujadili mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.
Katika mkutano huo wa siku mbili
wataalamu hao watajadili wautangaze ugonjwa wa Ebola kuwa janga la kidunia.

No comments:
Post a Comment