![]() |
| Marais wa Afrika baadaya kumaliza kikao na Rais Obama |
SIKU tatu za mazungumzo yaliyolenga mustakabali wa bara la Afrika
yamemalizika mjini Washington Marekani.
Mkutano huo ulikuwa wa kwanza wa
aina yake kati ya Marekani na viongozi wa Afrika na ulilenga kuimarisha
uhusiano kati ya Marekani na bara la Afrika.
Lakini kwa sasa mkutano umekamilika
, nini kimefikiwa ? Nani amefaidika na kwa njia gani?
Viongozi wanajiandaa kundoka mjini
humo na kwa mara nyingine kuongeza msongamano wa magari mjini DC.
Marais 40 wa Afrika walikwenda
Marekani kuona kile ambacho Rais Obama alikuwa amewaitia katika jitihada zake
za kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Afrika.
Waliondoka nchini humo wakiwa na
mikataba ya uwekezaji ambapo makampuni ya Marekani yameahidi kuwekeza katika
nchi zao.
Mikataba hiyo ni ya thamani ya dola
bilioni 14 pamoja na ahadi ya Marekani kuimarisha uchumi na mataifa ya Afrika
pamoja na mchango mwingine wa pesa ili kuimrisha miundo mbinu na upatikanaji wa
kawin barani humo.

No comments:
Post a Comment