![]() |
| Rais wa Iran Hassan Rouhan |
RAIS Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran itaendelea kuenzi damu ya mashahidi wake kwa kutosalimu amri na kusimama imara mbele ya madola ya kibeberu na watenda jinai wa kimataifa wanaotaka kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.
Rais Rouhani aliyasema hayo jana jioni katika hadhara ya maulamaa na wasomi wa mkoa wa Chaharmahal Bakhtiyar huko Magharibi mwa Iran. Amesema taifa la
Iran ndilo kubwa na lenye nguvu zaidi zaidi katika eneo hili na litaendelea kuyasaidia mataifa ya Iraq, Syria na Lebanon katika mapambano yao dhidi ya ugaidi na vilevile taifa la Palestina katika mapambano yake dhidi ya jinai za Wazayuni.
Rais Rouhani amesema kuwa maulamaa na wasomi wanabeba risala na majukumu mazito kutokana na matukio ya kusikitisha yanayolikumba eneo lote la Mashariki ya Kati. Amesisitiza kuwa hali hiyo inaonesha kuwa tunapaswa kuwa macho mbele ya njama za mabeberu dhidi ya Iran na eneo zima la Mashariki ya Kati.

No comments:
Post a Comment