![]() |
| Sehemu ya Mlima Kilimanjaro |
WATAALAMU wa mazingira wameeleza kuwa asilimia 80 ya theluji ya mlima Kilimanjaro
imetoweka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu.
Wataalamu hao
wameeleza hayo mapema jana mjini Moshi , mkoani
Kilimanjaro wakati wakiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa
kimataifa wa watalaamu wa sayansi ya mazingira unaotarajiwa kufanyika mwishobni
mwa mwezi August.
Wamesema njia
pekee ya kukabiliana na hali hiyo ni kuzuia ujkataji wa mito na kudhibiti
vyanzo vya maji vilivyopo kando yam lima huo mkubwa barani Afrika sanjari na
kuendesha kampeni maalum ya upandaji wa miti inayohifadhi mazingira.

No comments:
Post a Comment