SHIRIKA la chakula na kilimo duniani (FAO)
limeeleza kuwa zaidi ya watu milioni 150 barani Afrika wanakabiliwa na njaa
sugu(chronic hunger) kutokana na sababu mbalimbali lakini kunwa zikiwa ni vita
na ukame.
Katika
ripoti yao ya hali ya chakula na kilimo duniani ya mwaka 2012,wataaalamu hao wa kilimo na
uchumi toka FAO wameeleza kuwa katika nchi za jangwa la sahahra hali ni mbaya zaidi kutokana bna
sababu kuu mbili zilizotajwa hapo juu
Mbali na
hayo lakini sera mbovu na utawala mbovu wa serikali nyingi za Afrika katika
kutoa kipaumbele katika kuboresha kilimo sanjari na kuwawezesha wakulima ni
miongoni mwa mambo yanayochangia hali hiyo.

No comments:
Post a Comment