Saturday, August 9, 2014

WATAFITI waeleza kuwa ekari moja ya muhogo inazalisha Tshs milioni kumi na tano


Wafanyabiashara wa muhogo wakiwa sokoni

MBINU hafifu za kuwashawishi wakulima wa zao la muhogo wa mikoa ya Lindi na Mtwara imetajwa kuwa ni miomgoni mwa mambo yanayochangia umaskini wa kipato katika mikoa hiyo.

Wakulima wa zao la muhogo toka mkoani Mtwara wameeleza hayo mapema jana katika mahojiano maalum na waandishi  wa habari wakati wakisheherekea siku ya wakulima nchini maarufu kama nanenane .
Wamesema watafiti wa zao hilo wanaeleza kuwa ekari moja ya muhogo inazalisha shilingi kumi na tano elfu za kitanzania , lakini umaskini wa kipato kwa wakazi wengi wa mikoa ya Mtwara na Lindi ni kiwango cha juu pamoja na kuwepo kwa mazingira mazuri ya kuzalisha zao hilo.

No comments:

Post a Comment