Friday, September 19, 2014

BAN KMOOIN akutana na waziri wa nje wa Iran


Waziri wa nje wa Iran(kushoto)na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Kimoon(kulia)

WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, Iran ina azma thabiti ya kutatuliwa miradi yake ya nyuklia inayofanyika kwa malengo ya amani.

Akizungumza na Ban  Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Dakta Muhammad Javad Zarif amesema kuwa, serikali ya Tehran ina mtazamo mzuri kuhusiana na kupatikana makubaliano ya mwisho kati yake na kundi la 5+1.
Akizungumzia uhusiano kati ya Iran na nchi jirani na hasa serikali mpya ya Iraq, Dakta Zarif amesema kuwa, Iran iko tayari kutoa msaada wowote wenye lengo la kupatikana amani katika eneo, uhusiano mzuri na majirani na kusaidia mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi.
Kwenye mazungumzo hayo, naye Ban Ki moon amesema kuwa, Iran ni nchi yenye taathira kubwa katika eneo na inaweza kuwa na nafasi muhimu katika kutatua matatizo mbalimbali ya kieneo na kimataifa






No comments:

Post a Comment