Tuesday, September 9, 2014

DIWANI wa Chadema amtunuku tuzo ya uongozi mkuu wa wilaya Kilombero


Mkuu wa wilaya Kilombero Hassan Masala akipewa nishani
DIWANI wa kata ya Mngeta kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema) Felisian Kigawa amemtunuku tuzo ya uongozi uliotukuka Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala kwa usimamizi bora ulioharakisha maendeleo kata na tarafa ya Mngeta na wilaya hiyo kwa jumla.



Sambamba na Dc.Masala wengine waliopata tuzo na vyeti ni pamoja na Padre Egfrid Tonz alipata tuzo nne ikiwemo ya mchngo mkubwa wa maendeleo tarafani humo,kampuni ya KP,Mkurugenzi mtendaji wa wilayani humo na Camfed walipata tuzo mojamoja.

Tuzo hizo zilizotolewa mwishini mwa wiki zilikwenda sambamba na hafla ya uzinduzi wa  vyumba viwili vya maabara katika shule ya sekondari Kiburubutu vilivyojengwa kwa hisani ya DEZA kupitia serikali ya Uswiss likiwa ni ombi la Padri Tonz wa kanisa katoriki parokia ya Mchombe wilayani humo.

Kwa mujibu wa diwani Kigawa wazo la tuzo kwa mkuu huyo wa wilaya linatokana na ombi la wanachi kumpendekeza apate tuzo hiyo kutokana na kuthamini mchango wake kwa wanachi hasa anavyotumia muda wake kukabili changamoto zinazo wakabili.
Kuhusu Padri Tonz, Kigawa alisema kwa muda mrefu amekuiwa chachu ya maendeleo yanyoonekana na kukua kwa kasi hasa ikizingatiwa amekuwa akiiwezesha tarafa hiyo kujikwamua na changamoto za kimsingi katika kuelekea kwenye maendeleo.










No comments:

Post a Comment