![]() |
| Asakari wa wanyma pori wakishuhudia ujangili wa wanyama |
WAZIRI
wa
Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Lazaro Nyalandu amesema kuwa, ujangili nchini humo bado
unaendelea kushuhudiwa licha ya kuweko juhudi za kupambana nao.
Amesema hayo mjini Dar es Salaam katika mkutano wa
wadau wa maendeleo ya kupambana na ujangili na kusisitiza kwamba, kunaendelea
kufanyika juhudi za kubuni mbinu ili kukomesha vitendo hivyo.
Waziri Nyalandu amesema mkutano huo ni mwendelezo wa
mkutano uliofanyika Mei mwaka huu ukilenga kuwasilisha utekelezaji wa
makubaliano waliyoafikiana kila taifa ili kuona namna gani watasonga mbele
katika kukabiliana na viendo vya ujangili.
Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania amesema kuwa, moja ya hatua walizochukua ili kupambana na vitendo
vya ujangili katika mbunga za wanyama ni kuajiri askari wanyamapori 430 na hadi
Septemba mwaka huu wamelenga kupata askari 900.

No comments:
Post a Comment