Tuesday, September 9, 2014

MANISPAA za Ilalam na Morogoro zazindua mpango wa kutokomeza tatizo la ajira

Jengo la manispaa ya Ilala,jijini Dar
MANSPAA ya Ilala Jijini Dar es salaam na Manispaa ya Morogoro zimezindua program maalumu kutokomeza tatizo la ajira kwa vijana na wanake zikitumia sheria kuu na ndogo kuanzisha vitengo mbalimbali ikiwemo ya Mazingira na Afya kukabili changamoto hiyo na umasikini katika makundi hayo.
Program hiyo iliyobatizwa jina la ujirani mwema kwa maendeleo imeanza kwa kuhusisha kata ya Kichangani  Morogoro yenye mitaa 10 wakazi zaidi 12,400 na Ilala zikijikita kutumia vikundi mbalimbali vya kijamii na rasilimali zilizo kwenye kata kukabili changamoto hiyo ya ajira na Mazingira kutokana na kufanana.

Akizindua program hiyo katika ofisi ya kata Kichangani baad ya kupanda miti ya ushirikiano baina wanamazingira Ilala na kikundi cha MUWAKIMO Kichangani Morogoro,Diwani John Waziri aliahidi kutoa robo ya pato kwa kikundi kitakachojitokeza kuitekeleza sheria ndogo yenye adhabu ya shilingi 50,000.


Kwa upande wake Afsa mazingira manispaa ya Ilala Francis Gowele na mwenyekiti wa wanamazingira hao Khamisi Jaffari walisema manispaa zinaweza kukabili changamoto zinazowazunguka kama zitakuwa tayari kugawana na wananchi kupitia vikundi pato litokana nalo na kodi,adhabu na ushuru wa miji hiyo.


No comments:

Post a Comment