WENYEJI
Hispania Jumatano hii wanapambana na
bingwa wa ulaya Ufaransa na Brazil inakutana na Serbia kwenye mechi zilizosalia
za robo fainali ya mashindano ya mpira wa kikapu ya kombe la dunia mjini
Madrid, Hispania.
Matumaini ya Serbia kuangusha Brazil ni haba, asema kocha wao
Sasha Djordjevic ambaye ameisifu sana timu ya Brazil, akisema ndiyo bora zaidi
kwa zote kushiriki mashindano ya kiwango hiki.
Katika mechi ya makundi Brazil ilishinda Serbia 81-73.
Mechi kati ya bingwa wa Ulaya Ufaransa na Hispania itakuwa na
kukata na shoka baada Hispania kuibwaga Ufaransa 88-64 mechi za makundi.
Katika mechi za Jumanne usiku za robo-fainali Lithuania,
washindi wa shaba mashindano yaliyopita walishinda Uturuki 73-61 na kufuzu kwa
nusu fainali ambapo watakutana na bingwa mtetezi Marekani walioichapa Slovenia
119-76.
Mechi za nusu-fainali ni kesho na Ijumaa. Uturuki ilishinda
medalio ya fedha m,ashindano yaliyopita nchini Uturuki.

No comments:
Post a Comment